Akaongeza kuwa “Prugram inavipengele vingi, miongoni mwake ni utoaji wa mihadhara yenye anuani isemayo (Mahitaji ya mwanaadamu kinafsi na kiroho), imetolewa na Dokta Shaimaa Nasoro, mbobezi wa tiba za kisaikolojia na urekebishaji wa tabia, ameongea kuhusu mahitaji muhimu ya nafsi ambayo huleta ulingano na utulivu wa nafsi ya mtu”.
Akaendelea kusema “Kulikuwa na kipengele cha (Picha na maoni), kimeongozwa na Kawakibu Abdusataar, ameongea namna ya kuamiliana na mambo ya kiofisi katika mtazamo wa kimalezi, mada hiyo imepata mjadala mkubwa kutoka kwa washiriki”.
Kituo cha utamaduni wa familia kitaendelea na program hii kila wiki, ni sehemu ya mkakati wa kuwajenga watumishi waweze kupambana na changamoto za kinafsi katika maisha yao, kwa mujibu wa maelezo ya Hafaar.